
Siasa Za Kiwakati Za Ethnografia, Urithi, Na Maambukizi Katika Kipindi Cha Covid-19 Nchini Tanzania
Dondoo ya Mtoaji: Makala hii ni ya nne katika mfululizo wetu wa sehemu tano unaoitwa “COVID-19: Views from the Field.” Bonyeza hapa kusoma utangulizi ulioandikwa na mtengenezaji wa mfululizo huu, Rebekah Ciribassi. Kuhusu tafsiri: Tafsiri hii isingewezekana bila msaada wa msingi wa Sophia George, lakini kama kuna makosa ya kiuandikaji ni ya mwandishi. Shukrani ya dhati kwake. Nimeishi Tanzania tangu mwezi wa tatu mwaka 2018, nikiwa nafanya utafiti wa kiethnografia na familia mbalimbali ambazo zina wagonjwa wenye ugonjwa wa kurithi wa damu unaoitwa siko seli. Nilianza kuvutiwa na utafiti huu wa maisha ya kijamii na ya kisiasa kuanzia mwaka wa 2012, nilipojifunza kwa mara ya kwanza kuhusu kundi la wanaharakati wa kisayansi wa Pan-Afrika, pamoja na Watanzania, wanayoipa kipaumbele huduma na utafiti wa ugonjwa wa siko seli barani kote Afrika. Nilitaka kujua: mabadiliko gani ya msingi ya kianthropolojia yanatokea ili kuhamisha nyakati za maingilio ya afya ya dunia kutoka kasi (read more...)